Bao la Chama lampagawisha Waziri

Muktasari:

Makamba alisema bao la Chama dakika za jioni akimalizia kazi nzuri ya Haruna Niyonzima ilimpa furaha ya ajabu jana usiku ambayo hakuitarajia kwani aliamini Simba ilishatolewa CAF

Dar es Salaam. Soka ni burudani bwana! Unaambiwa bao la Clatous Chama limempgawisha Waziri wa wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Januari Makamba aliyedai Mzambi amemkosha.

Makamba alisema bao la Chama dakika za jioni akimalizia kazi nzuri ya Haruna Niyonzima ilimpa furaha ya ajabu jana usiku ambayo hakuitarajia kwani aliamini Simba ilishatolewa CAF.

Makamba aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mchezo huo mara baada ya kumalizika alisema bao la Chama lilimfanya ashindwe kuzuia furaha yake na kuanza kushangilia huku akiwa haamini nini kimetokea dakika hizo za mwishoni mwa mchezo.

“Lilikuwa bao muhimu ambalo Watanzania wote tumelifurahia, kile ndicho tulichokifuata uwanjani, nitoe pongezi zangu za dhati kwa mashabiki wa soka waliojitokeza kuishangilia Simba.

“Nimeona namna ambavyo muda wamingi walikuwa wakipiga kelele za kuwapa nguvu wachezaji wetu ambao pamoja na kutanguliwa walipambana na wakakomboa bao na kluongeza la ushindi,” alisema Mheshimiwa huyo.

Naye aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alikuwa miongoni mwa wanasiasa waliokunwa na matokeo ya juzi ya Simba.

Akitumia mtandao wake wa kijamii wa Twitter kuposti picha ikimuonyesha mnyama Simba akipanua mdomo.