Aussems apiga hesabu nusu fainali Ligi ya Mabingwa

Muktasari:

Simba imekata tiketi ya kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo mwaka 2003.

Dar es Salaam.Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema baada ya kikosi chake kupata ushindi katika mechi dhidi ya AS Vita katika mechi ya mwisho ya hatua ya makundi sasa akili na mipango yao ni kufanya vizuri katika hatua ya robo fainali.

Katika msimamo wa Kundi 'D' Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba walimaliza katika nafasi ya pili wakiwa na pointi tisa huku vinara wakiwa ni Al Ahly ambao walimaliza na pointi kumi.

Aussems alisema wachezaji wangu wamejituma kadili ya uwezo wao tulifungwa goli la mapema ila hatukukata tamaa tuliendelea kupambana hadi dakika ya mwisho malengo yalikuwa kufuzu makundi tulifanikiwa.

"Sasa tumefanikiwa robo tunajipanga kwa ajili ya kupambana kufuzu nusu fainali huu ni ushindi wa wana Simba wote, kwa Watanzania wote na hata kwa Afrika Mashariki hili ni jambo kubwa sana kwetu," alisema.

Kocha wa AS Vita, Florent Ibengé alisema tumefungwa na Simba naimani tumefungwa kutokana na wachezaji wa Simba kucheza katika ubora wao na sisi kucheza chini ya kiwango.

"Nampongeza kocha wa Simba, Aussems ni mjanja sana huyo nimesoma naye pamoja kule Ufaransa naimani ataifikisha mbali zaidi timu yake kikubwa Simba walikuwa bora zaidi yetu hivyo kwetu tunajipanga kwa msimu ujao," alisema Ibenge.