VIDEO: Kabasele aruka kimanga kula unga

Monday March 11 2019

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam. Mwimbaji wa bendi ya Akudo Impact, Alain Kabasele amefunguka kuhusu madai ya kutumia dawa za kulevya na kupoteza muelekeo katika muziki wake.

Kabasele mtoto wa aliyekuwa mwanamuziki Pepe Kale amesema anawasikia watu wanaomzungumzia kuwa anakula unga hajielewi, sasa anawauliza watu hao hajielewi vipi mbona haokoti makopo wala hajageuka kuwa chizi?

"Hizi habari nimeanza kuzisikia toka muda mrefu, kuwa mimi nakula unga, mara nimekuwa sijielewi napoteza mvuo katika uimbaji, mara nimekuwa kama chizi, sasa mbona siokoti makopo?

“Mbona hapa umenikuta na tunaongea vizuri? mimi najielewa na wala sili unga, sema watu wanaongea na kumpima mtu kwa macho tu," amesema  Kabasele

Aidha Kabasele amesema watu wamezoea maneno yeye hawezi maneno, hivyo kama ingekuwa kweli anatumia unga, hiyo ni starehe ya mtu mbaya ni kupitiliza hivyo watu waache kufuatilia maisha ya watu.

Advertisement