Rais Kenyatta amfuta kazi Waziri wa michezo Kenya, Balozi Amina achukua mikoba

Friday March 1 2019

 

By FADHILI ATHUMANI

Nairobi, Kenya. Waziri wa michezo wa Kenya, Rashid Echesa amefutwa kazi, kwa mujibu wa mabadiliko ya baraza la mawaziri, lililotangazwa leo, Ijumaa Machi mosi, na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Rais Kenyatta amemteua aliyekuwa Waziri wa Elimu, Balozi Amina Mohammed kuchukua nafasi ya Echesa.

Echesa, ambaye uongozi wake katika ofisi kuu ya michezo nchini, katika uongozi huu wa Rais Kenyatta imedumu kwa muda mfupi wa mwaka mmoja, anaondoka huku akiwa hana rekodi nzuri ya utendaji kazi.

Safari ya Echesa katika ya michezo haikuanza vizuri kwani mara baada ya kuteuliwa, alianza kuandamwa kashfa nyingi ikiwemo maswali kutoka kila kona, wengi wakihoji Elimu yake na sifa zilizopelekea uteuzi wake.

Advertisement