Julio aipa deni Serengeti Boys

Muktasari:

Jinsi kikosi cha Serenegti Boys kilivyo na ubora, hadhani kwamba Nigeria itafurukuta pindi timu hizo mbili zikikutana mechi ya ufunguzi, Aprili 14.

KOCHA wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ametamba fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitakazofanyika nchini mwezi Aprili, ni sehemu sahihi kwa vijana wa Tanzania wenye umri kama huo ‘Serengeti Boys’ kumfuta machozi kwa kuwafunga vijana wa Nigeria.

Machozi hayo ni yale ya timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka23 ya Tanzania, kutupwa nje na Nigeria katika mashindano ya kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana wa umri huo mwaka 2011 zilizofanyika Morocco.

Katika mchezo wa kwanza, Tanzania iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lakini ilichapwa mabao 3-0 ugenini huko Nigeria na kushindwa kufuzu fainali hizo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Julio alisema kwa jinsi kikosi cha Serenegti Boys kilivyo na ubora, hadhani kwamba Nigeria itafurukuta pindi timu hizo mbili zikikutana mechi ya ufunguzi, Aprili 14.

“Mashindano haya yangekuwa yanachezwa kwa mtindo wa mechi za nyumbani na ugenini, ningekuwa na wasiwasi kwa sababu Nigeria wamekuwa na kampeni za kihuni na fitina mno pindi wanapocheza kwao ili wapate matokeo, wafuzu. Lakini kwa vile yanachezwa hapa, siamini kama watatusumbua kwa sababu hawatapata nafasi ya kufanya hivyo.

“Kingine kinachonipa imani kubwa ni kwamba tuna timu nzuri ambayo haina woga wa kucheza dhidi ya timu yoyote ile. Wito wangu kwa Watanzania ni kuungana kuhakikisha timu inafanya vizuri. Tuweke kando utofauti wetu wa kiitikadi na tuwape sapoti vijana