Kocha Simba awaita mashabiki Iringa

Muktasari:

Awali jana Ijumaa baada ya mchezo wa Simba dhidi ya Azam, kocha huyo alisema, wamepita kwenye wiki ngumu lakini yenye furaha kwao.

Dar es Salaam. Kocha wa Simba Patrick Aussems amesema siku kumi zilizopita zimekuwa nzuri kwao kutokana na kwa kupata matokeo mazuri.

Amesema pia timu imeonyesha kiwango kizuri na mashabiki kufurahia wakati wote.

Hata hivyo licha ya mafanikio hayo yote, amesema jambo kubwa la muhimu ni mashabiki wa kujitokeza kwa wingi mkoani Iringa na Shinyanga kwa ajili ya kuipa sapoti timu hiyo kwa michezo yake inayofuata.

Kocha huyo aliandika ujumbe huo kwenye mtandao wake wa Twitter huku akiwaomba mashabiki hao kujitokeza kwa wingi uwanjani timu itakapokuwa ikicheza.

Awali jana Ijumaa baada ya mchezo wa Simba dhidi ya Azam, kocha huyo alisema, wamepita kwenye wiki ngumu lakini yenye furaha kwao.

 Aussems amesema, walicheza mechi ngumu ya Yanga na hii ya Azam FC lakini anashukuru wameshinda.

Kocha huyo maarufu kwa jina la Uchebe kutokana na staili yake ya kufuga ndevu ndefu kidevuni mwake amesema, baada ya michezo hiyo imeshapita, wanarudi kama kawaida kufanya maandalizi ya mchezo ujao.