Bale anaoa kwa mbwembwe kibao

Monday February 18 2019

 

Madrid,Hispania. Hii sasa sifa. Supastaa, Gareth Bale ameamua kukodi kisiwa na askari kibao wa kulinda usalama wakati atakapofunga ndoa na mrembo Emma Rhys-Jones, ambaye ni mama wa watoto wake watatu.
Bale ameamua kupeleka sherehe hizo za harusi huko kwenye kisiwa cha Tagomago kilichopo kwenye bahari ya Mediterranian, ambako ndiko alikomvisha pete ya uchumba. Uamuzi wa kupeleka harusi hiyo huko ni kwa ajili ya kuhakikisha usalama. Bale, anayelipwa Pauni 600,000 kwa wiki kabla ya makato ya kodi huko Real Madrid sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na vitisho vya kiusalama.
Wageni watakaoalikwa kwenye harusi hiyo hawazidi 150 ambao watakwenda kufurahia sherehe kwenye kisiwa hicho, ambacho ukikodi kila saa moja unalipa Pauni 500. Kwa sababu harusi hiyo itakuwa ya watu wachache, Bale na mama watoto wake wamedai kwamba watafanya sherehe nyingine huko Cardiff ili na kuwaalika wale ambao watakuwa wamekosa sherehe ya mwanzo. Harusi hiyo itafanyika mwishoni mwa msimu huu.

Advertisement