Bushiri: Mbao imejipanga vizuri kuikabili Yanga

Muktasari:

Mbao FC itakipiga na Yanga Jumatano ya wiki hii katika mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa kwenye Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza.

Mwanza.Wakati Mbao FC wakijiandaa kuwakabili Yanga katika mchezo wao keshokutwa Jumatano, Kocha Ally Bushiri 'Benitez' amesema wataingia kwa tahadhari kubwa katika mchezo huo.

Yanga itakuwa mgeni wa Mbao FC katika mchezo huo wa Ligi Kuu utakaopigwa kwenye Uwanja Kirumba jijini hapa.

Kocha Benitez alisema wataingia kwa tahadhari kubwa katika mchezo huo kwani wanajua wapinzani wao wametoka kupoteza mchezo uliopita.

Alisema Yanga watakuja kasi kubwa katika mchezo huo ili kupata ushindi jambo ambalo washajua jinsi ya kukabiliana nao.

Alisema wanataka kuendeleza rekodi yao ya kuwafunga Yanga katika mchezo uwanja huo hivyo wamejiandaa kikamilifu kushinda mchezo huo.