Ulimwengu afunga bao la kwanza Algeria

Muktasari:

Mshambuliaji Thomas Ulimwengu wa JS Saoura amefunga goli lake la kwanza katika timu hiyo tangu asajiliwe.

Dar es Salaam.Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu amefunga bao moja na kuisaidia timu yake ya JS Saoura kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi DRD Tadnejnat katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Algeria.

Mshambuliajia huyo wa zamani wa TP Mazembe, hakuwa katika wakati mzuri kwa hivi karibuni baada ya kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.

Katika mchezo huo Ulimwengu alianza kutupia goli la kwanza dakika 82 na kuinua mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo huku goli la pili likifungwa na Boukbouka dakika 90 na mchezo ukimalizika 2-0.

Kuanza kufunga kwa mshambuliaji huyu kumeanza kutoa taswira nzuri kwake baada ya mashabiki wengi kuona kama amepunguza kasi kwenye kutupia wavuni.

Kwa upande wa pacha wake Mbwana Samatta ambaye anakipiga katika klabu ya KRC Genk huku akiongoza kwa mabao (19) katika Ligi Kuu Ubeligiji.