Takwimu za wachezaji wa Yanga, Simba walivyocheza

Muktasari:

Katika  mchezo huo kulikuwa na ushindani mkubwa kati ya wachezaji wa timu zote mbili na makocha wa timu zote mbili

Dar es Salaam.Pambano la Watani wa Jadi jana Jumamosi lilikata maneno ya mashabiki wa soka vijiwezi ambao kila aliyekuwa anshabikia Simba au Yanga aliamini wataondoka na pointi tatu.

Katika  mchezo huo kulikuwa na ushindani mkubwa kati ya wachezaji wa timu zote mbili na makocha wa timu zote mbili.

Makala haya inakuletea alama za kila mchezaji na makocha alivyopata kutoka na michezo huo ulivyokuwa na alivyocheza.

Aishi Manula - 6

Muda mwingi alionekana akiwa anadaka mipira ya kawaida kwani hata mashambulizi ambayo walikuwa wakifanya Yanga hayakuonekana kuwa na mazara langoni mwake.

Manula alirahisishiwa kazi na mabeki wa Simba ambao waliweza kuwakaba vizuri mastraika wote wa Yanga. Katika alama Manula atapata sita kwani muda mwingi hakuwa katika misukosuko ya kushambuliwa.

Zana Coulibaly - 7

Ameonekana kuwa bora katika mechi hii kuliko ambavyo wengi walitarajia kutokana na uwezo alionesha katika kikosi cha Simba tangu alivyofika hapa nchini.

Coulibaly alikuwa bora katika kukaba, kuanzisha mashambulizi na kupiga krosi za maana ambazo kama mastraika wangekuwa makini wangeweza kufunga bao.

Kutokana na alivyocheza na uwezo alionesha anapata alama ya saba, na katika miongoni mwa wachezaji walionesha uwezo mzuri katika machi hii ya Dabi Coulibaly ni miongoni mwao.

Mohammed Hussein 'Tshabalala' - 5

Beki wa kushoto wa Simba alikuwa katika nafasi nzuri haswa timu inapokuwa inashambulia.

Lakini muda mwingine alikuwa akionekana si mzuri katika kukaba kwani upande wake ulikuwa ukitumika kupigwa krosi na wachezaji wa Yanga.

Tshabalala muda mwingine alikuwa katika kiwango cha chini katika kukaba na kuwachezea Boxer na Tambwe rafu, katika alama napata tano.

Pascal Wawa - 8

Kadri siku zinavyozidi kwenda akiwa ndani ya kikosi cha Simba amekuwa akionesha kiwango bora haswa kuwazuia mastraika.

Wawa aliens kumzuia Makambo na Tambwe ambao aliweza kuwapokonya mipira mingi na hata kuzuia mipira ambayo ilikuwa inaelekea kwao.

Katika kukana kwake Wawa alionesha uzoefu na ukomavu wa mechi kubwa kama dhidi ya Yanga kutokana na kiwango kizuri alichoonesha na katika alama anapata nane.

Juuko Murshid - 5

Alianza katika kikosi cha kwanza mbali ya kuwa anauguza majeruhi ya muda ambayo aliyapata katika mechi iliyopita ya Kimataifa dhidi ya Al Ahly.

Juuko alikuwa anakaba vizuri, katika mipira ya vichwa na hata kuonesha ubabe wake katika mipira ya kugombania.

Lakini pindi alipokuwa anapokonya au kuokoa mpira kuwa wakati alionekana akibutua pengine alikuwa hakiogopa kujitonesha maumivu yake na katika alama anapata tano.

James Kotei - 8

Alikuwa roho ya kiungo cha Simba kwani alitimiza vyema majukumu yake ya kwanza ya ukabaji kwa kuweza kuwazuia viungo wa Yanga Feisal na Tshishimbi kutokuleta madhara langoni kwao au kutawala mpira.

Kotei muda mwingine alikuwa bora katika kuanzisha mashambulizi lakini kwa uwezo wake mkubwa katika mechi hii ya Watani anapata alama nane.

Cletus Chama - 4

Mbali ya kuonesha soka safi katika kikosi cha Simba tangu alivyojiunga nacho msimu huu lakini katika mechi ya jana hakuwa katika kiwango chake bora. Chama alikiwa akipoteza mipira mingi na hata kushindwa kupiga pasi zake za mwisho.

Kutokana na kiwango alichoonesha katika mchezo wa jana anapata alama nne, na hata kipindi cha pili kilivyoanza alifanyiwa mabadiliko alitoka na kuingia Hassan Dilunga.

Jonas Mkude - 6

Alicheza vizuri katika eneo la kiungo mshambuliaji mbali ya kuzoeleka kuwa anacheza nafasi ya kiungo mkabaji.

Aliweza kupora mipira na kuwazuia viungo wa Yanga kutokuleta madhara katika eneo la kiungo ambalo ndio lilikuwa roho ya timu zote mbili.

Mkude ambaye ni miongoni mwa wachezaji walikuwa katika mechi waliocheza michezo mingi ya Dabi anapata alama sita.

John Bocco - 5

Nahodha wa Simba alikuwa akiwafanya muda mwingi mabeki wa kati wa Yanga Ninja, Yondan na Dante kutokupanda mbele na kuwa makini dhidi yake.

Hakupata nafasi ya wazi ya kufunga lakini alikuwa akisafa na kusumbua walinzi wa Yanga na katika alama anapata tano.

Meddie Kagere - 8

Alikuwa akisafa na kutafuta mipira mingi dhidi ya ngome ya ulinzi ya Yanga ambayo ilionekana kuwa makini tofauti na mechi tano zilizopita kwenye ligi.

Bao ambalo alifunga kipindi cha pili alionekana kucheza vizuri kwa kuelewana na Bocco ambaye alitoa pasi ya mwisho na katika alama anapata nane kwani mbali ya kufunga alicheza vizuri.

Kabla ya dakika mbili kumalizika alitoka na kuingia Haruna Niyonzima ambaye kwa muda aliocheza anapata alama moja.

Emmanuel Okwi - 6

Katika kipindi cha kwanza hakuwa na mchezo mzuri kwani alionekana akipoteza mipira mingi na kukabwa kwa uraisi na walinzi wa Yanga.

Kipindi cha pili Okwi alibadilika na kuwasumbua walinzi wa Yanga haswa Boxer ambaye muda mwingi alionekana kumkaba ingawa hata kuchezewa rafu.

Okwi alianza kuonekana kipindi cha pili kwa kuwasumbua walinzi hao wa Yanga ingawa faulo na hata mipira yake haikuwa na hatari zaidi na katika alama anapata sita.

YANGA

Ramadhani Kabwili - 5

Kipa wa Yanga hakuonekana kama anaweza kuimili ukubwa wa michezo huu wa Dabi lakini alicheza vizuri.

Kabwili hakuwa akishambuliwa mara kwa mara.

Mbali ya kufungwa Kabwili alikuwa imara muda mwingi kulingana na presha ya mechi ilivyokuwa na katika alama anapata tano.

Poul Godfrey 'Boxer'  - 5

Beki wa kulia wa Yanga ulikuwa michezo wake wa pili wa Dabi lakini kipindi cha kwanza alikuwa mzuri katika kukaba na kuzuia mashambulizi upande wake.

Boxer alifanikiwa kipindi cha kwanza kutokana upande wake alikuwa anacheza na Chama ambaye hakuwa katika kiwango kizuri.

Boxer kulingana na uwezo wake alionesha kuwa mzuri kwenye kukaba mbali ya kipindi cha pili kuzidiwa, lakini katika kushambulia alionekana kupoteza mipira na hata kupiga krosi ambazo zilipotea na katika alama anapata tano

Gadiel Michael - 5

Alianza vizuri kipindi cha kwanza kwa kuwazibiti washambuliaji wa Yanga, lakini hakuwa mzuri pounding timu inapokuwa inashambulia.

Michael kabla ya kutolewa na kuingia Matheo Anthony alikuwa katika kiwango cha kawaida pengine

kutokana na timu yao kuzidiwa.

Katika alama anapata tano, huku Anthony ambaye aliingia kipindi cha pili nae hakuonekana kubadili mchezo na Yanga muda wote walikuwa bado wakizidiwa.

Anthony nae katika alama anapata nne, kutokana na alivyocheza kwani muda mwingi alikuwa akipokea mipra ambayo haikuwa na madhara hata muda mwingine kupoteza na kukubali kubwa kwa uraisi.

Kelvin Yondan - 6

Beki wa kati wa Yanga ndio alike roho ya ulinzi katima kikosi cha timu hiyo kwani mbali ya kufungwa alikuwa akiwakaba vyema mstraika wa Simba.

Yondan alikuwa akiwakaba na kuwafanyia vurugu Bocco na Kagere ambaye alipata nafasi ya kufunga bao. Katika alama Yondan anapata alama sita.

 

Andrew Vicent 'Dante' - 5

Alikuwa akicheza kwa maelewano na Yondan lakini hakuwa katika kiwango bora kwenye kukaba kama alivyozoeleka dhidi yake.

Dante hakuwa mzuri katika mipira ya vichwa na hata muda mwingine alionekana kuzidiwa na kubutua mipira ambayo iliwafanya Simba kuendelea kushambulia, na katika alama anapata tano.

Abdallah Shaibu 'Ninja' - 7

Mbali ya kuzoeleka kama mlinzi wa kati lakini alicheza katika nafasi ya kiungo mkabaji kama alivyokuwa katika mechi ya mzunguko wa kwanza.

Ninja aliweza kuzuia mshambulizi mengi ya Simba ambayo kabla ya kuwafikia mabeki wa Yanga alike akihusika katika kukaba.

Uwezo wake wa kukaba washambuliaji wasumbufu kama Bocco, Kagere na Okwi iliendelea kuonesha ingawa kuna muda alike akicheza rafu na kubutua mipira bila ya sababu na katika alama anapata saba.

Feisal Salum.  - 6

Kiungo mshambuliaji wa Yanga alikuwa katika wakati mgumu kwani viungo wa Simba waliweza kuwa imara katika eneo hilo na kuzidiwa.

Salum muda mwingi likuwa akipiga pasi za pembeni ambazo hazikuwa na msahada kwenye timu na hata zile ambazo alike akipiga kwenda mbele zilikuwa zikinyakwa.

Katika kucheza alicheza vizuri kwa upande wa Yanga na katika wachezaji waliofanya vizuri ni mjongoni mwao na anapata alama sits.

Kabamba Tshishimbi - 5

Hakuwa akionekana muda mwingi katika kupora mipira au kuanzisha mashambulizi kutoka na nafasi yake ya kiungo mkabaji ambayo alikuwa anacheza.

Tshishimbi alizidiwa na viungo wa Simva na kukubali kukabwa kwa urahisi na Mkude ambaye alimnyima uhuru wa kufanya hatari langoni mwa Simba na katika alama anapata tano.

Heritier Makambo - 5

Kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga akifunga mara 11, alifanya shambulizi la hatai kipindi cha kwanza ambayo alipiga shuti nje ya boksi lilikwenda karibu na lango.

Tangu hapo walikubali kukabwa kwa urahisi na mabeki wa kati wa Simba, Wawa ambaye alionekana kumuweza sana. Makambo katika alama anapata tano.

Amissi Tambwe - 4

Alicheza kipindi cha kwanza tu, kabla ya kufanyiwa mabadiliko, lakini nae alikubali kuwa chini ya ulinzi wa mabeki wa Simba na kushindwa kufurukuta au kufanya jambo lolote la hatari.

Tambwe ambaye alishawahi kucheza Simba katika alama anapata nne kutokana na kiwango chake cha kawaida alichoonesha katika mchezo huo huo ndani ya dakika 45, alizocheza.

Baada ya kutoka Tambwe aliingia Ngassa ambaye nae hakuweza kunadilu mpira na hata alipokuwa anapata mipira au kutoa pasi zilikuwa hazina madhara yoyote kwa upande wa Simba.

Ngassa kwa kiwango alichoonesha nae anapata alama nne.

Ibrahim Ajibu 6

Nahodha wa Yanga ni mzuri katika kutengeneza nafasi za kufunga na hata kufunga mwenyewe lakini katika mechi ya jana walikubali kuwa chini ya ulinzi wa mabeki wa Simba ambaye walihakikisha hakuwa na madhara.

Ajibu alionekana muda mchache timu ilipouwa na mpira na hata muda mwingine hupoteza mipira hiyo, na sehemu nyingine ambaye ni bora katima mipira ya fault ambayo katika mechi na Simba hakupiga faulo au kona nzuri na zote zilikolewa wa walinzi wa Simba.

Ajibu alitoka na kuingia Mohammed Issa ambaye nae muda mwingi alikuwa alike mipira akiwa chini mbali ya lango la Simba.

Simba walikuwa bora katika eneo la kiungo baada ya kuingia Dilunga na hata Issa hakuwaweza kufanya lolote na katika alama anapata nne.