Failuna ashinda mbio za nyika Taifa

Saturday February 16 2019

 

By Bertha Ismail

Kilimanjaro. Mwanariadha Tanzania, Failuna Matanga ameshinda mashindano ya mbio za Nyika Taifa akitumia muda wa dakika 34:55 katika umbali wa kilomita 8 leo Jumamosi mkoani Kilimanjaro.

Mashindano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Gofu mjini Moshi, nafasi ya pili imeenda kwa mwanariadha Magnalena Shauri aliyetumia dakika 35:20 huku nafasi ya tatu akichukua Angelina Daniel Tsere aliyetunia dakika 36:45.

Nafasi ya nne imechukuliwa na Amina Mohamed (37:12), akifuatiwa na Marselina Issa (38:04) huku wa sita akichukua Rosalia Fabian (38:24).

Washindi sita wamechaguliwa kuingia kambini katika kambi ya taifa inayojiandaa na mashindano ya dunia ya mbio za nyika nchini Denmark.

Advertisement