Nyie, Wawa hachezi na majukwaa

Muktasari:

Kama ninavyosema kazi yangu najua kwa kuifanya ni uwanjani na si kubishana na mashabiki

Dar es Salaam.PASCAL Wawa kumbe ana madongo, kwani beki huyo wa kati wa Simba, amesema hafanyi kazi zake uwanjani na majukwaa badala yake kutimiza wajibu wake uwanjani na kwamba hana mchecheto na pambano lijalo la watani.
Beki huyo ambaye kwa sasa anacheza nafasi hiyo pamoja na Juuko Murshid raia wa Uganda baada ya Erasto Nyoni kupata majeraha ya goti.
"Kazi yangu ni uwanjani sio kuzungumza na mashabiki, ndio maana sipendi kuzungumza mengi nje ya uwanja kuhusu kazi yangu bali naiacha miguu yangu iongee nao," alisema Wawa alioyewahi kuichezea Azam Fc na El Merreikh ya Sudan.
Simba ilipofungwa mfululizo mabao 5-0 na AS Vita na Al Ahly ugenini, wadau wengi wa Simba walizungumza juu ya kiwango cha mchezaji huyo.
"Kama ninavyosema kazi yangu najua kwa kuifanya ni uwanjani na si kubishana na mashabiki," alisema Wawa.
Alisema, wao ni watekelezaji wanakwenda kujiandaa anachoamini watafanya vizuri katika mchezo huo: "Ni mchezo mgumu lakini si mara ya kwanza, tumejiandaa na tunakwenda kwa maandalizi mengine zaidi."
Simba na Yanga zinavaana Februari 16 keshokutwa, Uwanja wa Taifa katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ni wa mzunguko wa pili.