Aguero aivunja rekodi Shearer, Man City yapiga sita Chelsea

Muktasari:

Chelsea hii ni mara ya kwanza inapata kipigo kikubwa tangu walipofunga mwaka 1991, na sasa ipo nafasi ya sita na kujiweka katika wakati mgumu wa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.

Manchester, England. Mshambuliaji Sergio Aguero amefikia rekodi Allan Shearer ya kupiga hat trick 11, akiiongoza Manchester City kuichakaza Chelsea kwa mabao 6-0 kwenye Uwanja wa Etihad

Mshambuliaji Aguero ameweka rekodi ya kufunga hat-trick ya pili katika mechi tatu alizocheza na kuiongoza Manchester City kurudi kileleni kwa Ligi Kuu.

City ilikuwa mbele kwa mabao 4-0 katika dakika 25 za kwanza, Raheem Sterling alifunga bao la kwanza kabla ya Aguero kufunga bao la pili kwa shuti la umbali wa mita 30.

Aguero alifunga bao tatu akimalizia mpira uliorudishwa nyuma na beki wa Chelsea, Ross Barkley naye Ilkay Gundogan alifunga bao tatu kwa shuti la umbali wa mita 18 kabla ya mapumziko.

Aguero alifikia rekodi ya Alan Shearer ya kufunga hat-tricks 11 katika Ligi Kuu England akifunga penalti kabla ya Sterling' kuhitimisha kwa kufunga bao la sita.

Wakati Aguero anakwenda kuchukua mpira mwamuzi Mike Dean aliuficha mpira huo nyuma hadi alipomkaribia ndipo aliutoa mgongoni na kumpa.

Mshambuliaji huyo wa Argentina alikosa bao akiwa yeye na goli kabla ya kuweka rekodi yake ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Manchester City akiwa amefunga mabao 160 na kuivunja rekodi ya Eric Brook aliyekuwa amefunga mabao 158.

City sasa inaongoza ligi kwa tofauti ya mabao tisa kwa Liverpool, wenye mchezo moja mkono.