CAF yairudisha Ismaily Ligi ya Mabingwa

Muktasari:

Ismaily ipo kundi C sambamba na timu za TP Mazembe, Club Africain na CS Constantine

Shirikisho la Mpira wa Soka Afrika limeirudisha kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika timu ya Ismaily ya Misri.

Timu hiyo awali iliondolewa kwenye hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mashabiki wake kufanya vurugu kwenye mchezo wa raundi ya pili ya hatua hiyo dhidi ya Club Africain kutoka Tunisia.

Mashabiki hao walianzisha vurugu hizo kama njia ya kuonyesha kutofurahishwa na kitendo cha Club Africain kupata penati mbili zilizoifanya iibuke na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ismaily.

Uamuzi wa CAF uliotangazwa leo umefafanua kuwa rufaa iliyokatwa na Ismaily imekubaliwa na timu hiyo inarudishwa katika mashindano.