Tambwe, Tshishimbi ndani JKT Tanzania mjipange

Muktasari:

Yanga inashuka uwanjani kwa lengo la kupata ushindi dhidi ya JKT Tanzania ili kujiweka vizuri katika msimamo kabla ya kuivaa Simba.

Dar es Salaam. Baada ya kukosa michezo miwili ya Ligi Kuu kutokana na kuugukia jeraha mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe amerudi rasmi na anatarajia kuanza leo dhidi JKT Tanzania kwenye Mkwakwani, Tanga saa 10 jioni.

Tambwe aliumia katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Biashara Union ambapo timu yake ilifanikiwa kutinga hatua ya 16 bora baada ya kuitoa timu hiyo kwa mikwaju ya penalti 5-4.

Kwa mujibu wa kikosi cha timu hiyo kilichotolewa na benchi la ufundi nyota wawili waliokuwa wanaamzia benchi Tambwe na Papy Kabamba Tshishimbi wote wanaanza katika kikosi cha kwanza leo.

Katika michezo yote ya Ligi aliyocheza Tambwe msimu huu amekuwa akianzia benchi na akiingia amekuwa akibahatika kuisaidia timu yake kupata ushindi kama ilivyokuwa dhidi ya Tanzania Prisons alitokea benchi aliingia na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Kikosi cha Yanga kitakachoanza leo Ramadhani Kabwili, Paul Godfrey, Gadiel Michael, Andrew Vicent, Abdallah Shaibu, Papy Tshishimbi, Feisal Salum, Mrisho Ngasa, Ibrahim Ajib na Pius Buswita, Amiss Tambwe.