Buku 2 tu utaziona Simba, Yanga Taifa

Muktasari:

Leopards wana fainali wa msimu wa kwanza wa michuano hiyo ilitua asubuhi ya leo wakati wapinzani wa Yanga kwa msimu huu wa 2019, Kariobang waliwasili nchini alasiri hii wakiwa na mzuka wa kuendeleza kile walichokivuna kwenye Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.

AFC Leopards na Kariobang Sharks zote kutoka Kenye zimeshawasili nchini tayari kukinukisha kwenye michuano ya tatu ya S[portPesa Super Cup, lakini unaambiwa kama wewe ni shabiki na una buku mbili (Sh 2,000) unaziona Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Leopards wana fainali wa msimu wa kwanza wa michuano hiyo ilitua asubuhi ya leo wakati wapinzani wa Yanga kwa msimu huu wa 2019, Kariobang waliwasili nchini alasiri hii wakiwa na mzuka wa kuendeleza kile walichokivuna kwenye Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.
Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano wa SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya timu nyingine kutoka Kenya, Bandati FC itawasili alfariji ya leo huku watetezi Gor Mahia wenyewe watatua siku ya ufunguzi wa michuano hiyo, yaani Januari 22.
Aidha Sabrina alisema viingilio vya mechi hizo zitakazochezwa kati ya Jan 22-27 kile cha juu kabisa ni Sh 10,000 kwa Jukwaa la VIP A, huku VIP B na C ni buku tano tu na mzunguko ni buku mbili tu yaani Sh 2,000.
"Maandalizi yanaendelea vyema kwani timu zimeanza kuwasili kwa ajili ya msimu wa tatu wa michuano hiyo," alisema Sabrina.

Summary:
GOR Mahia wametwaa taji la Sportpesa Super Cup kwa misimu miwili mfululizo tangu michuano hiyo ilipoasisiwa mwaka 2017, ilianza kwa kuifunga AFC Leopards kwa mabao 3-0 katika fainali iliyopigwa Uwanja wa Taifa kabla ya mwaka jana kuichapa Simba 2-0 mjini Nakuru, Kenya."

HABARI ndio hiyo