Alliance yalazimisha sare kwa Prisons

Muktasari:

Licha ya timu zote kushambuliana na kutengeneza nafasi za mabao, lakini umakini katika kufunga ulikuwa mdogo na kusababisha dakika 90 zikimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mwanza. Tanzania Prison imefanikiwa kuondoka na pointi moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Alliance FC katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa leo Jumanne kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.

Timu hiyo iliyoanza msimu vibaya kwa sasa inapambana vikali kusaka pointi tatu ili kujinasua nafasi za mwisho na kukwepa rungu la kushuka daraja.

Katika mchezo huo ambao ulionekana kuwa na ushindani, Prison licha ya kutangulia kupata bao kupitia kwa Bashiru Ismail dakika ya 16, lakini wapinzani wao walisawazisha dakika ya 41 kupitia kwa Hussein Javu.

Kipindi cha pili kilianza huku kila timu ikionyesha dalili za kupata bao lakini umaliziaji ulikuwa tatizo pande zote na kujikuta wakigawana alama moja moja.