Mbwana Samatta awawaza Romelu Lukaku,Roberto Firmino

Muktasari:

Mbwana Samatta awawaza Romelu Lukaku,Roberto Firmino. Baba mzazi wa staa huyo, Ally Pazi Samatta amelimegulia siri Mwanaspoti Online kwamba mpaka sasa Ujerumani kuna timu mmoja, Uingereza zipo tano ikiwemo Evarton na Newcastle, Hispania mbili na Uturuki moja.

PENYE nia pana njia ndivyo ilivyo kwa mshambuliaji wa kimataifa, Mtanzania Mbwana Samatta anayekipiga Genk ya Ubeligiji, anaweza siku moja aje acheze na mastaa wa Ulaya Romelu Lukaku (Man United) na Roberto Firmino (Liverpool).
Hilo limekuja baada ya uwepo wa timu nyingi zinazohitaji huduma yake ikiwemo Uingereza ambako klabu tano zinamtaka baadhi ni Everton na Newcastle.
Baba mzazi wa staa huyo, Ally Pazi Samatta amelimegulia siri Mwanaspoti Online kwamba mpaka sasa Ujerumani kuna timu mmoja, Uingereza zipo tano ikiwemo Evarton na Newcastle, Hispania mbili na Uturuki moja.
"Anatamani kucheza Uingereza hasa ndoto yake ni kupata nafasi Man United na Liverpool, hivyo anatafuta daraja kwa hizo timu zinazomtaka huko kama Everton na nyinginezo.
"Hivi karibuni aliongeza mkataba wa mwaka mmoja na nusu kwenye timu yake ya Genk, nia ya viongozi wake ni kutaka kumuuza kwa gharama ya juu.

"Kifupi mwezi huu itajulikana kama ataenda wapi lazima litimie na kipou mbele chake ni Uingereza kama haitakuwa hivyo ataenda timu yoyote itakayofika dau la klabu yake ya sasa,"anasema.