Tukitathimini ya mwaka 2018,tujipange 2019

Saturday January 5 2019

 

By Ali Mayay

Ni  dalili  ya kuwa  na  heri na  baraka kwetu sote ambao   leo hii tumepata  nafasi ya kupitia makala hii  ikiwa  ni jumamosi ya kwanza  ndani ya  mwezi wa kwanza   wa  mwaka  2019 wakati wapo wenzetu wengi  tunaowafahamu na  tusiowafahamu ambao tulikuwa nao mwaka uliopita lakini  kwa mapenzi ya Mungu hawakupata bahati ya kuuona  mwaka huu ambao  kwa mujibu  wa kalenda tunayoitumia ya Gregori  (Gregorian calendar) ni mwaka 2019.
Kwa kuwa kutoka mwaka mmoja kwenda  na kufika mwaka mwingine ni mafanikio katika maisha  hivyo ni   kawaida   kwa mwanadamu kuyafurahia mafanikio ingawa yapo mafanikio ambayo  mwanadanu  anaweza kujivunia kutokana na mchango wake katika kuyafikia  mafanikio hayo lakini yapo  mafanikio mengine  ambayo manadamu  hawezi kujivunia kutokana  nakutokuwa na mchango wowote katika kuyafikia mafanikio hayo. Miongoni mwa mafanikio ambayo mwanadamu huwa hana mchango wake ni  hiki ninachokizungumzia hapa  yaani  ni kufanikiwa kuwa hai na afya njema kama hivi tulivyo leo huku tukiwa tunapata makala ya kwanza kabisa kwa mwaka huu tukiwa salama.
Kwa kadiri miaka inavyozidi kusonga mbele  ndio  watu huweza kujitathmini  viwango vya maendeleo  katika  mambo wanayoyafanya  katika maeneo yao  ya kazi   ndio maana  ukiona  mtu  anasherehekea   kuuaga  au kuukaribisha  mwaka   fulani basi ujue mtu  huyo  ana kitu cha kijuvunia  katika mwaka huo.Ndio maana  ukienda katika kumbukumbu za historia za timu ya Manchester United ya nchini Uingereza utasikia  pamoja na mafanikio waliyoyapata  lakini lazima  wanataja darasa la mwaka 1992 (Class of 1992).   Sababu gani  mwaka huo unatajwa ? tu kwa sababu ndio mwaka  vijana sita walifaulu kutoka  katika timu ya vijana na kujiunga na kikosi hicho ambacho kilipata mafanikio makubwa kwa kutwaa vikombe vitatu katika msimu wa mwaka 1998/1999. Hivyo    mwaka 1992 ukitajwa na Manchester United unaamisha  watu sita ambao ni David Beckham, Nicky Butt, Ryan Giggs, Gary Neville, Phil Neville na Paul Scholes.
 Kufanya tathmini kila mwaka unapoisha  ni  moja kati ya kitu kinachotakiwa kufanyika kuanzia ngazi ya wachezaji, makocha, vingozi na baadae washabiki kwani   kila mmoja ana   nafas I yake katik aeneo lake itakayoweza kumfanya akumbukwe hata kama hatakuwepo. Leo hii  tumekuwa  tukimtaja Peter Tino kwa kuwa ndiye aliyefunga goli dhidi ya Zambia lililotupeleka  Tanzania katika Fainali za Mataifa huru ya Afrika za mwaka 1980 zilizofanyika nchini Nigeria.
Naandika  kuwa jamii ya wanasoka Tanzia inatakiwa kutahmii kile tulichokifanya katika mchezo huu ili tuweze kujirekebisha  mwka unaofuata kwani mwaka huu 2019 tunatarajia kuwa wenyeji wa fainali za CAF  za vijana wenye umri chini  ya miaka 17 hivyo kuitumia fursa hiyo kuandika historia itakayokumbukwa na vizazi vijavyo. Lakini kuweka historia huwa hakuji hivi hivi bali huhitaji maandalizi  ambayo hufanyika baada ya kujitathmini  kama ambavyo tunatakiwa kuutathmini mwaka 2018 na soka la Tanzania.Miongoni mwa mafanikio ya mwaka 2018  ni timu yetu ya soka  Taifa  U-17 kushika nafasi ya pili katika mashindano ya U-17 katika ukanda wa nchi za cecafa  nyuma ya Uganda ambayo ilitwa ubingwa, timu hiyo hiyo ilitwaa , timu hiyo hiyo ya Vijana U-17 ilitwaa ubingwa wa mashindano hayo ya vijana kwa nchi za COSAFA ambayo iliakikwa katika mashndano hayo.  Kwa upande wa vilabu ni Simba kufanikiwa kuingia ktika hatua ya makundi kwenye michunaoi vya vilabu bingw abarabni Afrika.
Kwa upande wa pili  ambao unatakiwa kuangaliwa kwa makini  na kutafuta kilichosababisha  ni kuwa mwaka 2018 ndio mwaka timu yetu ya vijana wenye umri chini ya miaka 23  ilitolewa katika masindano ya CAF kwa vijana wenye umri huo, timu yetu ya Taifa ya wakubwa ilipoteza matumaini ya kushirii katika fainali za CAF za mwaka huu baada ya kupoteza mechi dhidi ya lesotho ambayo ilionekana kuwa  na wepesi wa  kupata  matokeo ukilinganisha na timu nyingine atika kundi letu. Lakaini pia  mwaka 2018  ndio mwaka ambao  ligi kubwa kabisa nchini  ya soka  yaani ligi kuu  ilimaliza mkataba wa udhamini  na mdhamini mkuu  hivyo ligi hiyo kuchezwa bila y kuw an mdamini  mkuu. Hivyo ni imani yangu kuwa wadau wote   tuliopo katka mchezo wa soka  kila mtu akijifanyia tahmini yake katika eneo linalomhusu kwa kuungalia mwaka 2018 kisha akajipanga kwa ajili ya mwaka huu 2019 naamini  yatakuwa ni mafanikio makubwa sana  kwa ujumla wake  hapo mbeleni!
Kwa leo naishi hapo huku nikisubiri mrejesho kutoka kwako.
 
 

Advertisement