VIDEO: Masau Bwire awatolea bastola mashabiki Yanga

Muktasari:

Tukio hilo limetokea badaa ya Ruvu Shooting kulala kwa mabao 3-2 kufuatia bao la dakika za mwisho ya mchezo.

Dar es Salaam.Katika hali ya kushangaza Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amelazimika kutoa bastola kuwatawanya mashabiki wa Yanga waliomvamia baada ya mchezo wa timu hizo.

Tukio hilo limetokea leo mara baada ya mchezo huo kumalizika ambapo mashabiki hao wa Yanga waliokuwa wakishangilia ushindi wao ghafla wakakutana na Bwire akiwa anaelekea eneo ambalo aliegesha gari yake.

Wakati mashabiki hao wakimzonga Bwire wakimdhihaki kwa timu yake kukubali matokeo mwisho msemaji huyo akionekana kubadilika kwa kuwa mkali.

Mashabiki hao wakiendelea kumfanyia dhihaka Bwire huku wengine wakichukua kumbukumbu ya picha kwa kukutana na Afisa Habari huyo maarufu.

Wakati tukio hilo likiendelea ghafla Bwire alijikuta akitoa bastola yake ubavuni kushoto kisha kuwatishia mashabiki hao na baadhi kutawanyika haraka na kukimbia.

Baada ya kutoa bastola hiyo Bwire alipata upenyo na kukimbilia katika gari yake huku akionekana kuchukizwa na tukio la kuzongwa na mashabiki hao.

Hata hivyo Afisa wa jeshi mstaafu Jamal Rwambo  alilazimika kumsihi Bwire kupunguza hasira kisha msemaji huyo kuondoka haraka eneo la kuegesha magari.