Kumbe Simba ilijipanga mapema

Muktasari:

Simba tumejipanga kwanza kufikia malengo yetu ya awali ya kucheza hatua ya makundi na baada ya hapo tutaweka malengo mengine ambayo naona tunanafasi kubwa ya kuyafikia pia.

Kitwe, Zambia. KIKOSI cha Simba kinatarajia kuwasili nchini alfajiri ya kesho Jumatatu kikitokea hapa Kitwe Zambia ambapo jana walicheza mechi ya duru la kwanza dhidi ya Nkana Rangers na matokeo kama ulivyosikia.

Kikosi hiko kilikuwa hapa Kitwe, kwa siku nne kuanzia Alhamisi mpaka Jumapili na walifikia katika hoteli ya The Milford ambayo ipo pembezoni mwa katika mwa Kitwa.

Simba waliandaliwa hoteli ya The Court na wenyeji Nkana kama sheria za CAF zinavyosema timu ngeni wanatakiwa kuandaliwa kila kitu na timu mwenyeji, lakini kwa wawikilisha hawa wa Tanzania mambo yalikuwa tofauti.

Msafara wa Simba uliokuwa chini ya Ofisa Mtendaji Mkuu  Crescentius Magori tangu ulivyofika hapa Kitwe ulijitafutia kila kitu na kujihudumia na kuachana na vile ambavyo waliandaliwa na Nkana.

Mwanaspoti iliweka kambi hapa Kitwe anakuletea mambo kadhaa ya maisha ya hapa ambayo maabingwa hao watetezi waliyapitia.

Gharama ya hoteli

Katika hoteli ya Milford ambayo Simba waliishi kwa siku zote hizo chumba kimoja kilikuwa Dola 80 si chini ya Sh 160,000 na mabingwa hao walichukua vyumba 25.

Hoteli hiyo ambayo ina madhari mazuri ambayo yalikuwa ya utulivu wa hali ya juu naa ukimya uliotawala hata usalama na ulinzi ulikuwa mkubwa mno.

Wachezaji na viongozi wa Simba walitegewa mahala maalumu ambapo walikuwa wanawekewa chakula, huku wateja wengine waliokuwa katika hoteli hiyo walikuwa na sehemu yao kula chakula.

Muda mwingi wachezaji wa Simba walionekana kujifungia katika vyumba vyao na kama alikuwa akionekana basi ni kwa shughuli maaalumu kama kula au kuongea na simu. 

Maisha ya hapa

Muda mwingi maisha ya hoteli ambayo waliofikia Simba mbali ya kuwa na ukimya lakini kulikuwa hakuna watu wanaokatiza ovyo katika hoteli hiyo pengine kutokana na ulinzi mkali uliokuwa hapo.

Maisha ya hapa Kitwe, kwa upande wa Simba walikuwa kama kivutia haswa pale kikosi cha Simba kilipokuwa kinakwenda uwanjani kufanya mazoezi au siku ya mechi mashabiki wengi walionekana wakipiga miruzi na shangwe kuishangilia timu hiyo.

Kikosi cha Simba kila walipokuwa wanakwenda mazoezini au siku ya mechi mbele kulikuwa na gari ya polisi ambayo ilikuwa ikikongoza kikosi hicho na hata madereva waliokuwa wanaendesha magari hapa walikuwa wakisimama nao wakishangaa msafara huo wa Simba.

Kiujumla kikosi cha Simba mbali ya kupokelewa katika mazingra salama na mazuri na Nkana, licha ya kuhitaji  kujihudumia wenyewe walikuwa wakiishi vizuri na kulikuwa hakuna hujuma walaa jambo lolote baya ambalo walifanyiwa na wapinzani.

Usafiri

Viongozi wa Simba waliokuwapa hapa Kitwe chini ya mkuu wa msafara Magori waliamua kuchukua basi kubwa ambayo kama yale ya kusafiri mikoani ambalo aina ya Zhontong na walitumia kwenda katika mazoezi na mechi.

Basi hilo ambalo lilikuwa na ragi ya njano na nyeusi kwa siku gharama yake kwa siku kuwapeleka Simba ilikuwa Dola 550 (zaidi ya Sh 1 Milioni ) kwa maana hiyo kwa siku nne ambazo Simba walikuwa hapa walilipa zaidi ya Sh 5 Milioni.

Katika basi hilo nyota wa Simba walionekana kujiachia huku wakisikiliza mziki na kuangalia luninga kubwa na vitu vyote hivyo vilikuwaa vinapatikana katikaa basi hilo.

Mashabiki waongeza mzuka

Mashabiki wa Simba walitua hapa Ijumaa usiku na walifika katika hoteli ya Milford ambayo kikosi cha timu hiyo iliweka kambi na waliongeza mzuka kwani wachezaji walitoka katika vyumba vyao na kuanza kusalimiana nao.

Mara baada ya kusalimiana wachezaji walirudi katika vyumba vyao na baada ya hapo mashabiki waliondoka na kwenda katika hoteli mbalimbali ambazo walifikia hapa Kitwe.

Jumamosi mchana saa 7:00 mashabiki walikuja katika hoteli huku wakiwa wanapiga ngoma kama wanavyofanya wakiwa Uwanja wa Taifa na mzuka ulikuwa kama umeamshwa upya kuelekea katika mechi. 

Mashabiki wa Simba walifika katika hoteli hiyo wakiwa na basi ambalo walikodiwa na uongozi wa Simba baada ya lile lao kupata ajali wakati wanakuja hapa Kitwe na basi hilo lilikuwaa na bendera ya Simba.

Kifupi ni kwamba mabosi wa Simba walijipanga mapema vilivyo pengine kuliko hata mchezo wao wa ugenini wa raundi ya awali dhidi ya Mbabane Swallows ambako waliibuka na ushindi wa mabao 4-0.