Prisons yavuta watatu kutoka Lyon

Muktasari:

Prisons inasajili kimya kimya na kusubiri kutanga wachezaji wao wapya baada ya kufungwa kwa usajili wa dirisha dogo kesho Jumamosi.

IMEBAKIA kesho tu, dirisha dogo la usajili kufungwa, Prisons ya Mbeya imenyakua wachezaji watatu wawili kutoka African Lyon, Adam Omary, Adam, Ibrahim Hamadi na Kassim Kalungo kutoa Zima Moto ya Zanzibar.
Viongozi wa Prisons wamekuwa na usiri sana kuweka wazi majina ya wachezaji hao wakisubiri hatua ya pili ya pingamizi itakayoanza baada ya kesho baada ya kufungwa dirisha hilo lililofunguliwa tangu Novemba 15.
Mwanaspoti linafahamu kwamba limemalizana na wachezaji hao na majina yao yalipelekwa jana Alhamisi TFF ili kusikilizia pingamizi kutoka kwa klabu ambazo walianza nazo msimu huu.
Alipoulizwa katibu wa timu hiyo, Abdallah Havimtishi kwamba wamewasainisha kwa miaka mingapi hao wachezaji! Alikuwa mkali kama mbogo akijua umesikia wapi taarifa hizo.
"Sio wakati wa kuwatangaza wachezaji wetu, dirisha likifungwa mtajua tu, hivyo sina lolote la kukujibu kuhusiana na hilo, kama utataka kujua maendeleo ya timu sawa nitakujuza,"alisema.
Kocha wa timu hiyo,  Abdallah Mohammed 'Bares' yeye alisema alishapeleka ripoti kwa viongozi ili waifanyie kazi, hivyo atakuwa tayari kuwapokea wachezaji ambao watamletea kufanya nao kazi.
"Ili mladi watanisajiliwa nafasi na sifa za mchezaji nilizotaka nitakuwa sina ubishi, lengo ni moja ni kuona Prisons inashinda mechi na kutoka nafasi mbaya tuliopo,"alisema.