VIDEO: Mabosi Simba wamaliza kila kitu Zambia

Thursday December 6 2018

 

By Doris Maliyaga

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Swedy Nkwabi amesema tayari wameshafanya maandalizi ya kutosha nje na ndani ya uwanja namna watakavyowakabili wapinzani wao Nkana ya Zambia.

Nkwabi aliyeongozana na kikosi cha Simba kutoka Eswatini kwa ajili ya kuwapa nguvu na baada ya kupata taarifa Nkana ndiyo watakaopambana nao mechi za raundi ya kwanza wakaanza kazi.

Akizungumza na MCL Digital, Nkwabi amesema: "Tumeshafanya maandalizi yote ya mchezaji huo tutakapofikia yaani kambi na malazi kwa ujumla, hadi tutakavyocheza mchezo wetu."

Amesema, kutokana na maandalizi hayo, Wanasimba wasiwe na wasiwasi kabisa juu ya mchezo huo kwa sababu kila kitu kinakwenda vizuri.

"Hata wa hapa Dar es Salaam vitu kama kambi na mambo mengine yote yako tayari," alisisitiza.

Advertisement