VIDEO: Magori: Simba tupo kamili kumaliza Mbabane

Muktasari:

Simba inashikiri kwa mara ya kwanza mashindano ya Ligi ya Mabingwa baada ya kukaa nje kwa takribani miaka mitano

Mbabane, Swaziland. Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori ametua na timu yake hapa Swaziland akisema kila kitu kipo sawa kwao kuelekea mechi dhidi ya Mbabane Swallows itakayochezwa kesho.

Magori amesema tangu wamefika jiji la Manzini ambako mchezo huo utapigwa wamekuwa katika tahadhari kubwa kukwepa hujuma zozote.

Magori amesema uongozi wao umekamilisha kila kitu kilichokuwa kinahitajika katika timu yao na sasa wanasubiri mchezo wenyewe.

Alisema akili yao ni kuhakikisha Simba inatinga hatua inayofuata kukamilisha malengo yao ya kutinga hatua ya makundi na kwenda kuchukua kombe la Ligi ya Mabingwa.

Magori ambaye ameongozana na mwenyekiti wa Simba, Sued Mkwabi na mjumbe wa bodi Mulamu Nghambi ameongeza kwamba wakiwa hapa uongozi wao umeridhishwa na maandalizi ya ndani ya uwanja kutoka kwa makocha wao.