Euro 2020: Ujerumani yatupwa Uholanzi, England yabebwa

Muktasari:

Timu mbili za kwanza kutoka kila kundi zinafuzu moja kwa moja huku timu nne zitakazopita kama washindi watatu bora itaangaliwana mafanikio yao katika mashindano ya Nations League.

London, England. Mabingwa wa zamani Ujerumani na Uholanzi watakutana katika mechi za kufuzu kwa Euro 2020, baada ya kupangwa pamoja katika ratiba iliyopagwa leo Jumapili jijini Dublin, huku England wakipewa kundi la timu tano.

Ujerumani ndiyo timu tishio zaidi katika kundi hilo pamoja na hivi karibuni kuwa na matokeo mbaya katika mashindano ya Nations League.

Timu mbili za juu kutoka katika makundi 10, zinafuzu kwa Euro 2020, fainali ambazo kwa mara ya kwanza zitafanyika katika nchi 12 tofauti barani Ulaya.

Kikosi cha Gareth Southgate kimepangwa Kundi A pamoja na Czech Republic, Bulgaria, Montenegro na Kosovo.

England imepagwa katika kundi la timu tano tofauti na wenzake zenye timu sita kwa sababu wamefuzu kwa nusu fainali ya Nations League, ambayo yatafanyika Juni mwakani nchini Ureno. Ratiba ya fainali hizo itapagwa kesho Jumatatu.

Mechi za kusaka kufuzu zitaanza kuchezwa Machin a kumalika Novemba 2019.

Makundi

Kundi A: England, Czech Republic, Bulgaria, Montenegro, Kosovo

Kundi B: Ureno, Ukraine, Serbia, Lithuania, Luxembourg

Kundi C: Uholanzi, Ujerumani, Northern Ireland, Estonia, Belarus

Kundi D: Uswisi, Denmark, Republic of Ireland, Georgia, Gibraltar

Kundi E: Croatia, Wales, Slovakia, Hungary, Azerbaijan 

Kundi F: Hispania, Sweden, Norway, Romania, Faroe Islands, Malta

Kundi G: Poland, Austria, Israel, Slovenia, Macedonia, Latvia

Kundi H: Ufaransa, Iceland, Uturuki, Albania, Moldova, Andorra

Kundi I: Ubelgiji, Russia, Scotland, Cyprus, Kazakhstan, San Marino

Kundi J: Italia, Bosnia and Herzegovina, Finland, Ugiriki, Armenia, Liechtenstein