Hadi mapumziko Uganda yaiweka njia panda Stars

Muktasari:

Uganda inatakiwa kushinda mchezo huo ili kuiweka Tanzania katika mazingira mazuri ya kusaka kufuzu kwa Afcon2019

Kampala, Uganda. Safari ya Tanzania kwenda Cameroon bado ngumu baada ya vinara wa Kundi L, Uganda kulazimishwa suluhu na Cape Verde hadi mapumziko kwenye Uwanja wa Nambolee, Kampala.

Kwa matokeo hayo Uganda bado inaongoza kundi ikiwa na pointi 11, huku Cape Verde ikishusha Tanzania hadi nafasi ya tatu kwa tofauti ya mabao baada ya kulingana kwa pointi 5, huku Lesotho ikiburuza mkia.

Uganda ikicheza mbele ya mashabiki wake ilitegeneza nafasi kadhaa kupitia kwa mshambuliaji wake Faruku Miya, lakini alishindwa kuzitumia.

Kipa wa Uganda, Denis Onyango alifanya kazi ya ziada kuokoa hatari kadhaa golini kwake na kufanya timu hizo kwenda mapumziko matokeo yakiwa sare 0-0.

Msimamo wa Kundi L hadi dakika 45

                           Pld       W    D     L      GF   GA   GD  Pts                         

1      Uganda       4        3      1      0      6      0      +6    11  

2      Cape Verde   4      1      1      2      4      4      0      5

3        Tanzania      4      1      2      1      3      4      −1    5             

4      Lesotho        4       0      2      2      2      7      −5    2

UGANDA IMEFUZU HIVI

Uganda katika mchezo huo ilicheza bila presha yoyote kwa sababu inajua inaweza kufuzu hata kama watapoteza mchezo huu dhidi ya Cape Verde:

Uganda inaongoza Kundi ikiwa na pointi 10, tano zaidi ya Tanzania. Cape Verde ipo ya tatu na pointi nne na Lesotho ikiwa ya mwisho na pointi mbili.

Kama Cape Verde itaifunga Uganda kwenye Uwanja wa Namboole, Blue Sharks watafikisha pointi saba 7, wakati Uganda itabaki na pointi 10. Hata hivyo Uganda inaweza kufuzu iwapo Tanzania itafungwa na Lesotho kesho mjini Maseru.

Sare kati mchezo wa Lesotho dhidi ya Tanzania itamaanisha Stars itafikisha pointi sita huku Lesotho wakiwa na pointi tatu hivyo hakuna kati yao atakayeweza kuipata Uganda.

Endapo Lesotho itaifunga Tanzania, wenyeji watafikisha pointi tano sawa na Tanzania wakiwa na mechi moja mkononi hivyo kuna yoyote kati yao anayeweza kuifikia Uganda ambayo hata ikifungwa na Cape Verde itakuwa na pointi zake 10.

 Njia nyingine ambayo Uganda inaweza kupita kwenda  Cameroon.

Iwapo mechi hii Uganda dhidi ya Cape Verde itakwisha kwa sare hiyo ni ishara kuwa si Cape Verde au Lesotho anayeweza kuifikia Cranes baada ya michezo yote. Jambo pekee linaloweza kutokea ni mechi ya kuamua nani awe kinara wa kundi kati ya Uganda na Tanzania.

Kama Uganda itashindwa kuifunga beat Cape Verde na Tanzania itaifunga Lesotho, bado wanaweza kufuzu katika mchezo wake wa mwisho kama atafanikiwa kuepuka kipigo Dar es Salam.

Uganda imejihakikishia kufuzu kwa asilimia 80, endapo hataifungwa mchezo huu, na kusubiri jinsi itakavyochukua nafasi ya kwanza.

Hata hivyo, Uganda anaweza kushindwa kufuzu iwapo atafungwa mechi hizi mbili, huku Cape Verde na  Tanzania wakishinda mechi zao mbili za mwisho.

 

Uganda Cranes XI:

Kipa: Denis Onyango (Mamelodi Sundowns), Nico Wakiro Wadada (Azam FC), Godfrey Walusimbi (Kaizer Chiefs), Murushid Juuko (Simba SC), Hassan Wasswa (El Geish), Denis Iguma (Kazma FC), Khalid Aucho(Church Hill Brothers), Faruku Miya (Gorica), Moses Waiswa (Vipers SC),  Patrick Henry Kaddu (KCCA FC), Isaac Muleme (Haras El Hodood),

Akiba:

 Jamal Salim (Al Hilal, Sudan), Nicholas Sebwato (Onduparaka FC, Uganda), Joseph Ochaya (TP Mazembe),Timothy Awanyi (KCCA FC, Uganda), Isaac Isinde (Kirinya-Jinja SS, Uganda), Ibrahim Sadam Juma (KCCA FC, Uganda), Tadeo Lwanga (Vipers SC, Uganda), Allan Kateregga (Cape Town City, South Africa), , Milton Karisa (MC Oujda, Morocco), Edrisa Lubega (SV Ried, Austria), Derrick Nsibambi (Smouha, Egypt), Allan Kyambadde (KCCA FC, Uganda)