VIDEO: Shangwe Stars laanzia Afrika Kusini

Muktasari:

Ushindi wa Stars dhidi ya Lesotho unaiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kufuzu kucheza AFCON mwakani, lakini ni iwapo Uganda itaibuka na ushindi dhidi ya Cape Verde leo

Jo’Burg, Afrika Kusini. Umati wa mashabiki wa Taifa Stars waishio Afrika Kusini na wale waliosafiri kwa basi  kutoka Dar es Salaam kwenda Lesotho, wamekutana kwenye kitongoji cha Yeovil jijini Johannesburg na kuanza shangwe tayari kwa safari ya kuelekea Lesotho asubuhi hii.

Mashabiki hao walikuwa wakishangilia kwa kuimba nyimbo mbalimbali kwa lugha ya Kizulu ambazo wameahidi ndizo zitatumika wakati wa kushangilia kwenye mchezo huo.

Katika staili hiyo ya kushangilia wamekuwa wakipiga miguu chini kuashiria kuwa wataikanyaga Lesotho.