Coastal Union waibomoa Singida United

Muktasari:

Beki Miraj Adam yupo mbioni kujiunga na klabu ya Coastal Union baada ya kuanza mazungumzo ya awali kuhusu kuitumikia klabu hiyo.

Dar es Salaam. Beki wa Singida United, Miraj Adam yupo mbioni kujiunga na Coastal Union akiwa mchezaji huru.

Kutokana na ukata unaendelea ndani ya kikosi cha Singida, beki Miraj alikaa chini na uongozi wa klabu hiyo na kufikia hatua ya kuvunja mkataba baada ya makubaliano ya pande mbili.

Mwanaspoti online inafahamu kuwa nyota huyo yupo jijini Daresalaam kwaajili ya mazungumzo na Mabosi wa Coastal Union, lakini hata hivyo Ndanda walionyesha nia ya kutaka saini yake.

Coastal Union inaonekana kuwazidi kete Ndanda kutokana na ukaribu waliokuwa nao na mchezaji huyo ambaye aliwahi kuichezea timu hiyo kabla ya kutimka Singida Utd.

Kinachochelewesha dili hilo kukamilika ni baada ya kuwa na vuta nikuvute katika upande wa maslahi.