Mutamba, Ovella kuongoza mashambulizi Kenya U23 v Mauritius, Moi Kasaran

Muktasari:

Kikosi kamili cha Kenya U23: Brian Bwire (Kipa), Yusuf Mainge, Johnstone Omurwa, Nahodha Joseph Okumu, David Owino, Chrispinus Onyango, Teddy Osok, Ibrahim Shambi, James Mazembe, Pistone Mutamba, Ovella Ochieng.
Akiba: Timothy Odhiambo, Mike Kibwage, Jafari Owiti, Sydney Lokale, Tobbias Otieno, Alwyn Tera, na Henry Ochieng

Nairobi, Kenya. Kikosi cha timu ya taifa ya Kenya, chini ya miaka 23, kinajitosa uwanjani Moi Kasarani, muda mfupi ujao kuwavaa Mauritius katika mtanange wa kusaka tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la mataifa ya Afrika (AFCON U23), ambapo Pistone Mutamba na Ovella Ochieng wataongoza mashambulizi.
Kwa mujibu wa kikosi cha Kenya U23, kilichowekwa hadharani muda mfupi na kocha mkuu wa timu hiyo, Francis Kimanzi, langoni atasimama Kipa wa Kariobangi Sharks, Brian Bwire, ambaye atawategemea mabeki Yusuf Mainge, Johnstone Omurwa, Nahodha Joseph Okumu na  David Owino.
Kwenye Kiungo, kama ilivyotarajiwa, Kimanzi atawatumia Teddy Osok na Ibrahim Shambi kuchezesha timu huku Crispinus Onyango akisimama nyuma ya Mutamba, wakati James Mazembe na Ochieng Ovella wakitumika kuisasambua beki ya Mauritius wakitoke pembeni na kumalisha mfumo wa 4-3-3.
Kikosi kamili cha Kenya U23: Brian Bwire (Kipa), Yusuf Mainge, Johnstone Omurwa, Nahodha Joseph Okumu, David Owino, Chrispinus Onyango, Teddy Osok, Ibrahim Shambi, James Mazembe, Pistone Mutamba, Ovella Ochieng.
Akiba: Timothy Odhiambo, Mike Kibwage, Jafari Owiti, Sydney Lokale, Tobbias Otieno, Alwyn Tera, na Henry Ochieng
Kikosi cha Mauritius: Alexandre Figaro, Adel Langue, GukoolaNeelesh, Vincent Emmanuel, Jean-Jacques Patate, Lionel Larose, Alison Charlot, Saramandif Kengy, Adrien Francois, Wilson Damien, Jason Ferre
Akiba: Pascal Ferre, Sophie Dawson, Jackson Fernando, David Igory, Mustafa Bilaal, Cataperman Ronaldo, na Richie Nani