VIDEO: Rayvanny ajisalimisha Basata kisa wimbo wa Mwanza

Muktasari:

Rayvany aliwasili Basata saa 5:30 asubuhi akiwa na gari nyeupe aina ya Toyota Harrier akiwa amesindikizwa na watu wawili mmoja akiwa ni meneja wake anayejulikana kwa jina la Luvanga.

Akiwa amevalia suruali nyeusi na sweta la rangi ya machungwa yenye kofia ambayo alijifunika hadi usoni.

Dar es Salaam. Siku moja baada ya wimbo wake wa Mwanza kufungiwa, msanii Rayvanny amejisalimisha katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

Rayvany aliwasili Basata saa5:30 asubuhi akiwa na gari nyeupe aina ya Toyota Harrier akiwa amesindikizwa na watu wawili mmoja akiwa ni meneja wake anayejulikana kwa jina la Luvanga.

Akiwa amevalia suruali nyeusi na sweta la rangi ya machungwa yenye kofia ambayo alijifunika hadi usoni.

Baada ya kufika hapo aliegesha gari kwa muda kabla ya kuelekea ofisi za Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Godfrey Mngereza.

Wimbo wa Mwanza ulifungiwa jana na Basata kwa kile kilichoelezwa kuwa tungo zake zinashawishi masuala ya ngono na unaenda kinyume cha maadili ya Mtanzania.