AIBU: Mata, Sanchez wacheka Man United ikipokea kipigo

Muktasari:

Wachezaji wanadai kuwa mashabiki wanaonekana kukatishwa tamaa na matokeo na mwenendo wa timu hiyo ambayo imefanya vibaya zaidi msimu huu ikiwa ni mara ya kwanza kupoteza mechi nne kati ya 12 za kwanza tangu msimu wa mwaka 1990-91.

Manchester, England. Wachezaji wawili wa Manchester United wamewashangaza mashabiki baada ya kuonekana wakicheka wakati timu yao ikipokea kipigo cha mabao 3-1 katika kwa Manchester City katika mchezo wa Manchester derby.

Alexis Sanchez na Juan Mata walionekana wakichekea chinichini wakiwa benchi dakika chache kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza.

Katika mchezo huo vijana wa Jose Mourinho walikubali kufungwa bao la mapema ndani ya dakika 12, wakati David Silva ilipofunga bao la kuongoza kwa City.

Pia, mabao ya Sergio Aguero na Ilkay Gundogan iliendelea kufanya siku mbaya kwa Man United katika mchezo ambao hawatausahau.

Hata hivyo bado picha zilionyesha Sanchez na Mata wakipata jambo la kuwafurahisha wakiwa benchi…

Manchester City ilitawala mchezo huo kwa asilimia 65% huku vijana hao wa Guardiola walionekana walikuwa na uwezo wa kufanya lolote dhidi ya wapinzani wao.