Harusi ya Tambwe kukaa jamvini tu

Saturday November 10 2018

 

By Doris Maliyaga

Dar es Salaam. Mambo ya Waarabu acha tu kama hujazoea yatakushinda ndicho kilichopo katika sherehe ya Mrundi Amissi Tambwe na mkewe Raiyan Mohammed kwa wageni wote kukaa chini kwenye majamvi.

Sherehe hii ambayo waalikwa ni wanawake na inafanywa kama ilivyokuwa wakati msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba anaoa Mombasa Kenya.

Tofauti ya hii ni kwamba wageni waalikwa wote wanakaa chini kwenye mazuria maalumu isipokiwa madijei na waimbaji wa bendi ya Halichachi Modern Taarabu.

Pia, wazazi wanawake wa Raiyan ambao wameshafika ukumbini hapa wametengewa viti viwili.

Mke wa Tambwe ni Mtanzania mwenye asili ya Arabuni na mambo yanavyokwenda ni kwa staili hiyo.

Baadhi ya waalikwa waliokwishafika ni wake wa wachezaji kama wa Beno Kakolanya.

Advertisement