Ulimwengu abwaga manyanga Al Hilal

Muktasari:

Ulimwengu hakuwa na namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Al Hilal tangu amejiunga nayo Mei mwaka huu.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu amevunja mkataba wake wa miaka miwili na klabu ya Al Hilal ya Sudan.

Ulimwengu alijiunga na Al Hilal baada ya kuachwa na klabu ya Elskistuna ya Sweden Mei mwaka huu.

Katika klabu hiyo ya Sudan, Ulimwengu alifanikiwa kucheza michezo kadhaa ya Ligi Kuu Sudan pamoja na Kombe la Shirikisho Afrika.

Hata hivyo, Ulimwengu hakuwa na namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Al Hilal.

Ulimwengu alijiunga na Al Hilal baada ya kukaa muda mrefu bila kucheza soka tangu aachane na timu ya AFC Eskilstuna ya Sweden aliyokuwa akiitumikia.

Winga huyo pia aliwahi kuichezea TP Mazembe pamoja na mshambuliaji Mbwana Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji kwa sasa.