#Uchaguzi Simba: Kimya cha tawala ukumbini

Muktasari:

Mara baada ya kumaliza ajenda zilizokuwa katika mkutano mkuu wanachama wa Simba waliingia katika hatua ya mkutano wa uchaguzi.

Dar es Salaam. Kimya kimetawala katika ukumbi wa Julius Nyerere wakati wanachama wa Simba wakisubiri kupata matokeo ya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo.

Mara baada ya wanachama kumaliza kupiga kura walitolewa nje ya ukumbi na kutakuwa kwenda nje.

Wanachama hao baada ya kutoka nje kuna ambao waliamua kuondoka majumbani mwao na wengine ambao wapo mpaka sasa.

Wanachama waliobaki hapa ukumbi wamegawanyika katika makundi matatu kwenye sehemu ambazo wamekaa.

Kundi la kwanza wapo ndani katika katika ukumbi ambao ni eneo kabla ya kuingia katika ukumbi wenyewe ambao unatumika katika zoezi la kupiga kura.

Wanachama waliokaa katika eneo hili mbali ya kukaa katika vikundi tofauti kuna ambao walikuwa wanaangalia Luninga ambayo ilikuwa ikionesha video za maisha ya wanyama.

Wengine wapo katika vikundi wakiangalia mechi ya Yanga dhidi ya Ndanda kupitia simu zao za mkononi na hata wengine pia waliangalia mechi kati ya Chelsea na Crystal Palace.

Wengine wapo nje ya jengo lakini ndani ya uzio wakiwa wamekaa katika vikundi tofauti wakijadili mambo yao.

Hao ambao wapo nje ya ukumbi, lakini ni ndani ya uzio wengine wamelala katika bustani wakisubiri kuhesabiwa kura limalizike.

Kundi la tatu wapo nje kabisa ya uzio wa ukumbi huu wamekaa katika vikundi wakijadili mambo yao.

Wanachama hawa waliokuwa nje kabisa wengine wapo wamelala katika magari yao (daladala) waliokuja nayo kama kikundi.

Makundi yote matatu yapo yakiendelea kujadili mambo yao na wengine kuhusu uchaguzi lakini ukimya umeendelea kuwa mkubwa mno.

Baadhi ya wanachama ambao waliondoka kuna wengine wakisikia kuwa wanaenda ila baadae watarudi kusikiliza matokeo ya uchaguzi.

Mbali na wanachama kuwa katika makundi hayo katkka ukimya na utulivu wa hali ya juu ulinzi pia umetawala.

Kabla ya kuingia ndani ya uzio wa ukumbi huu kuna askari polisi wakiwa nje na wamebaki gari zao mbili hapo.

Askari wengine wapo ndani ya uzio wakiwa wengine wapo ukumbini na hata katika chumba cha uchaguzi pia kuna wengine wapo wakiimalisha usalama.