Niyonzima naye ndani CAF

Muktasari:

Kaheza na Mo Rashid wamesajiliwa mdimu huu lakini hawana bahati ya kupata nafasi kubwa ya kucheza kutokana na nyota wengine waliopo ndani ya Simba.

Simba imepeleka majina ya kikosi kitakachoshiriki michuano ya kimataifa ya  Ligi ya Mabingwa Afrika yanayosimamiwa  na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika  (CAF)  ambapo kwenye kikosi hicho kuna la kiungo mnyarwanda Haruna Niyonzima .
Wakati jina la Niyonzima likitumwa CAF, majina ya washambuliaji wawili Marcel Kaheza na Mohamed Rashid yamewekwa pembeni ambapo sasa watalazimika kupambania namba kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Tanzania  bara.
Niyonzima hajacheza mechi nyingi za Simba hadi sasa, lakini jina lake limepelekwa kwa vile lilitumwa kwa muda mrefu wakiamini kwamba kiungo huyo atakuwa miongoni mwa nyota watakaoibeba timu hiyo msimu huu.
Hata hivyo, matarajio ya Simba yalikuwa tofauti kwani kiungo huyo ameshindwa kulishawishi benchi la ufundi na mara kwa mara amekuwa akirejea kwao Rwanda kwa kile kinachoelezwa kukerwa na kitendo cha kutopata nafasi ya kucheza.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya Simba kililiambia Mwanaspoti kuwa: "Hao wawili hawamo kwenye kikosi hicho ila Niyonzima hayumo kiundani zaidi watakuwa wanafahamu viongozi ila naamini ni kwa vile majina alitumwa muda mrefu".
Kwa upande wa Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' alikiri kutumwa kwa majina hayo akisema , "Yatatangazwa muda si mrefu kwani ni lazima watu wafahamu, hivyo kila kitu kitajulikana na kuondoa maswali yote, ila kwa ufupi watu watambue kikosi chetu tulikituma muda tu sana".