#UCHAGUZI SIMBA: Wanachama wamiminika ukumbini

Muktasari:

Wanachama wa klabu ya Simba wanazidi kujitokeza katika mkutano mkuu wa timu ambayo unafanyika hapa ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Dar es Salaam. Wanachama wa Simba wameendelea kumiminika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano Julius Nyerere utakapofanyika mkutano mkuu pamoja na uchaguzi wa klabu hiyo.

Awali mkutano ulipangwa kuanza saa 2:30 asubihi, lakini mpaka muda saa 3:55, ulikuwa bado hajaanza ila wanachama wanazidi kuongezeka.

Katika ukumbi huu kuna sehemu mbili za kukaa wanachama juu na chini na kwako muenekano waliokuwa chini wameshaanza kujaza.

Muda wowote kuanzia sasa kwa majibu wa mwananchama mmoja ambaye alikuwa akitoa matangazo alisema watafunga milango ya juu ili wanachama wakakae huko.

Nje ya ukumbi pia wanachama nao wanazidi kumiminika na kuweka misululu ya kuhakikisha kadi zao ili kuingia ndani ya ukumbi.

Mistari miwili ya wanachama ipo nje ya ukumbi ambayo kati yao kuna wanaohakiki kadi na wengine kulipia.