Derby ya Arusha huko Simba, Yanga zinasubiri!

Muktasari:

Uwanja wa Sheikh Amri Abeid  kila mmoja anautumia kama uwanja wake wa nyumbani, lakini siku hiyo Arusha United ‘Wana Utalii’ ndio wenyeji ambao wamesema hawatakubali kuwaachia wageni wao pointi za ugenini.

ARUSHA. Makocha wa timu za Arusha United na Arusha FC wako katika presha ya hali ya juu kuhakikisha hawapotezi alama hata moja katika uwanja wao wa Sheikh  Amri Abeid siku ya Jumamosi.

Mchezo huo wa watani mkoani Arusha unasubiriwa kwa hamu kama vile ya mechi ya Simba na Yanga, huku mashabiki wa kila upande wakitamba timu yao kuibuka na ushindi.

Fred Felex Minziro ni kocha mkuu wa kikosi cha wana utalii ‘Arusha United’ ambapo amesema kuwa atambana kufa na kupona kuhakikisha hapotezi pointi ya nyumbani tena kama ilivyotokea mechi iliyopita dhidi ya Boma FC ya Mbeya.

“Maandalizi yako vizuri na presha ya timu iko juu na tutapambana kufa na kupona kuhakikisha tunavuna pointi maana  hatuko tiyari kupoteza tena alama yoyote nyumbani kama ilivyotokea mechi iliyopita dhidi ya Boma fc hivyo makossa yote tumeyaboresha na hayatajitokeza tena.”

Kwa upande wake kocha msaidizi wa Arusha FC, David Nyambere amesema kuwa kikosi chake kiko vizuri na kina morali ya hali ya juu kuhakikisha wanavuna alama katika uwanja huo wanaoutizama kama nyumbani

“Jumamosi tunakaribishwa na ndugu zetu Arusha united katika uwanja ambao tunautizama kama wa kwetu hivyo hatutaki kuharibu nguvu tuliyoanza nayo ugenini namaanisha tutahakikisha tunashinda mechi hiyo.”