Cannavaro aaga Zanzibar kwa ushindi

Muktasari:

Katika mchezo huo Yanga iliwatumia wachezaji ambao hawakupata nafasi ya kucheza kipindi kirefu kama Hajji Mwinyi, Emmanuel Mwartine, Juma Abdul na Mzimbabwe Thaban Kamusoko.

Dar es Salaam. Mchezo maalumu kwa ajili ya kumuaga aliyekuwa beki na nahodha wa Yanga na Taifa Stars, Nadir Haroub 'Cannavaro' umewafanya vijana wa Jangwani waibuke na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Malindi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Cannavaro ambae amestaafu mwishoni mwa msimu uliopita na kupewa ubosi wa Meneja Mkuu Yanga. Alishafanyiwa tukio kama hilo mkoani Morogoro Uwanja wa Jamhuri na Dar es Salaam Uwanja wa Taifa sambamba na kumkabidhi beki Abdallah Shaib 'Ninja' jezi yake.

Mabao yao ya mchezo huo yalipachikwa dakika ya 44, na Emmanuel Martine akimalizia pasi ya Mrisho Ngassa ambaye alifanya kazi kubwa kutengeneza bao hilo.

Ngassa aliifuka tena dakika ya 60 na kufunga bao hilo la pili na ushindi akimalizia pasi ya Pius Buswita.

Katika mchezo huo ambao pia Yanga walitumia nafasi ya kuwachezesha wachezaji ambao hawakupata nafasi ya kucheza kwa kipindi kirefu kama Hajji Mwinyi, Mwartine, Juma Abdul na Mzimbabwe Thaban Kamusoko.

Yanga imepata nafasi ya kucheza mechi hiyo, baada ya kupata mapumziko ya muda kupisha mechi za timu za Taifa Stars.