Mo Rashid: Ipo siku nitaaminiwa Simba

Thursday October 11 2018

 

By Doris Maliyaga

Dar es Salaam.  Mshambuliaji wa Simba, Mohammed Rashid 'Mo Rashid' amesema, uzoefu wa wachezaji aliokutana nao Simba ndiyo sababu ya kuwa benchi.
Mo Rashid ambaye alikuwa na nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza 'first 11' cha Tanzania Prisons na hata akachaguliwa timu ya Taifa Stars.
Lakini, tangu ajiunge na mabingwa wa Ligi Kuu Bara Klabu ya Simba mwanzoni mwa msimu huu, hajapata nafasi ya kuanza zaidi ya kuingia katika dakika za mwishoni.
Amefafanua sababu kubwa ni namna ambavyo ushindani aliokutana nao kikosi hapo.
"Utafika wakati wangu wa kucheza na mimi nitapata nafasi kikubwa ni kujituma tu ili nije kuisaidia Simba. Kwa sasa kama unavyoona Simba ina wachezaji wengi hasa wenye uzoefu wa muda mrefu hata sisi tutacheza tu,"alisema Mo Rashid.
Simba inawatumia zaidi washambuliaji kama, Mnyarwanda Meddie Kagere, Emmanuel Okwi raia wa Uganda na John Bocco 'Adebayor' ambao wana uzoefu wa kutosha huku Mo Rashid na wachezaji wengine kama Adam Salamba na Marcel Kaheza wakisubiri.

Advertisement