Makonda: Kuna uwezekano waliomteka Mo wamepewa ushirikiano na Watanzania

Thursday October 11 2018

 

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema Jeshi la Polisi litafanya kazi usiku na mchana kuwasaka watekaji hao.
Pia amesema Kuna uwezekano wazungu hao wamepewa ushirikiano na watanzania, hivyo kwa yeyote atakayebainika pia akachululiwa hatua Kali.
Makonda ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa huo amesema hatua wanazochukua ni pamoja na kuanza ukaguzi wa hotel zote za mkoa wa Dar es salaam ili kupata taarifa za wageni wake katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Pia amesikitishwa na Siasa kuingilia kati agizo lake la kuorodhesha idadi ya wakazi wanaoishi katika kila mtaa ili kuwa na kumbukumbu ya taarifa zao.
Makonda aliyekuwa mmoja Kati ya watumiaji wa gym ya hotel hiyo amesema hatua iliyopo katika mpango wa kuimarisha usalama wa jiji hilo ni kufunga Kamera katika maeneo yote makubwa ya jiji hilo ikiwamo barabarani na mahoteli makubwa.

Advertisement