Wachezaji Simba wajazwa noti za mashabiki

Muktasari:

Kocha msaidizi wa simba masoud Djuma aondolewa rasmi Simba.

Kocha huyo ameshindwa kutokea uwanjani wakati timu yake ikicheza dhidi ya African Lyon. Katika orodha ya wachezaji wa Simba pia jina la kocha huyo halikuwemo

Nyota wa Simba, Mohammed Hussein na Maddie Kagere wameoga noti kutoka kwa mashabiki wa group Simba kwanza ikiwa Kama motisha kwa nyota hao ambao kila mmoja aliibuka mchezaji bora katika michezo ya ligi, Kagere katika mchezo dhidi ya Mwadui na Tshabalala katika mchezo wa jana Jumamosi dhidi ya Lyon.

Pengine ni muda uliopangwa kucheza kwa mechi kati ya Simba iliyoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya African Lyon ndio umesababisha msisimko wa mashabiki kuwa wa kawaida Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ni kawaida zikicheza klabu kongwe iwe Simba ama Yanga kujaza nyomi ya mashabiki wao, lakini kwa Wanamsimbazi leo imekuwa tofauti kidogo.

Mashabiki wapo lakini sio kama wanavyokuwa wanafurika na kuwafanya wachezaji wakifunga wanakuwa wanapagawa na staili ya kushangilia.

Mashabiki waliopo wanajitahidi kwa uwezo wao kupiga mavuvuzera na vigoma lakini sio kama ilivyotarajiwa wakati wa usajili wao wa mwanzo mwa msimu ambapo mashabiki hao walikuwa wana hamu ya kuona majembe yao yakifanya kazi.

Soma zaidi: