Kikosi cha Malkia Strikers kinachoenda Japan hadharani

Nairobi, Kenya. Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Kenya ya mchezo wa netiboli kwa kina dada, 'Malkia Strikers', Japheth Munala, ametangaza kikosi cha wachezaji 15, kitakachowakilisha taifa kwenye mashindano ya Dunia kwa wanawake, itakayofanyika kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba 20, nchini Japan.
Katika kikosi hicho kilichosheheni nyota kibao akiwemo Nahodha Mercy Moim, Trizah Atuka na Jane Wacu, Munala amewajumuisha wachezaji wawili wapya ambao ni Lorine Chebet na Sharom Chepchumba wote kutoka klabu ya Kenya Prisons, huku mzoefu Everlyene Makuto, akiachwa.
Wengine walioingia katika kikosi hicho pamoja na Jane Wacu na Janet Wanja ni pamoja na beki Elizabeth Wanyama na Agripina Kundu. Kwa mujibu wa Munala, timu hiyo itaweka kambi katika uwanja wa ndani wa taifa wa Moi Kasarani.

KIKOSI CHA MALKIA STRIKERS
Jane Wacu, Janet Wanja, Edith Wisah, Trizah Atuka, Lorine Chebet, Christine Siwa, Mercy Moim (Nahodha), Noel Murambi, Sharon Chepchumba, Leonida Kasaya, Violet Makuto, Agripina Kundu, Emmaculate Chemtai, Elizabeth Wanyama,

VIONGOZI:
David Kilundo (Meneja wa Timu), David Lungaho (Mkurugenzi wa ufundi), Japheth Munala (Kocha Mkuu), Josp Barasa (Kocha msaidizi), Josephine Wanza (Daktari wa Timu), Sarah Karonge (Kocha wa viungo).