Wadau waweka kiulizo Harambee stars itakayoivaa Ghana

Nairobi, Kenya. Kocha wa Harambee Stars, Sebastien Migne ametaja kikosi cha wachezaji 38, watakaowakabili Ghana, katika mechi ya kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Ubingwa wa Kombe la Mabara Afrika (2019 AFCON), itakayopigwa Septemba 8, mwaka huu.
Katika kikosi chake, Migne amewaita nyota 18 wa ndani na maproo 19 waliokuwa wanakipiga katika vilabu mbalimbali nje ya nchi, miongoni mwao akiwa ni pamoja na Masoud Juma, ambaye kwa sasa hana timu baada ya kutengana na klabu ya Cape Town City FC ya Afrika Kusini.
Kwa nyota wa Ndani, Migne amemjumuisha kikosini mlinda lango, Farouk Shikalo,  anayefanya poa kwenye KPL, msimu huu na klabu yake ya  Bandari. Mwengine aliyeitwa ni nyota wa zamani wa Azam FC ya Tanzania, Allan Wanga ambaye kwa sasa anakipiga Kakamega Homeboyz.
Hata hivyo, katika hali isiyotarajiwa wadau wa soka nchini wametoa dukuduku lao kwenye mitandao ya kijamii wakionekana kutoridhishwa na kitendo cha kukosekana kwa baadhi ya nyota kwenye kikosi cha Stars, akiwemo kiungo mchezeshaji wa Gor Mahia, Francis Kahata na mwenzake Humphrey Mieno.

Nyota wa ndani:

Makipa: Patrick Matasi, Boniface Oluoch, Brian Bwire, Farouk Shikhalo,

Mabeki: Philemon Otieno, Jockins Atudo, Dennis Odhiambo, Joash Onyango, Bernard Ochieng.

Viungo: Whyvone Isuza, Francis Kahata, George Odhiambo, Duncan Otieno, Samuel Onyango.

Straika: Cliff Nyakeya, Abdallah Hassan, Piston Mutamba, Allan Wanga, Masoud Juma.

Nyota wanaokipiga nje:
Abud Omar, Johanna Omollo (Cercle Brugge), Anthony Akumu, Jesse Were, David Owino (Zesco United), David Ochieng, Eric Johanna (IF Bromma), Ian Otieno (Red Arrows), Eric Ouma, Ovella Ochieng (Vasalund), Ismael Gonzalez (Fuenlabrada), Cliff Miheso (Buildcon), Musa Mohamed (Nkana FC), Joseph Okumu (Ann Arbor), McDonald Mariga, Michael Olunga (Kashiwa Reysol), Paul Were (FC Kaisar), Brian Mandela (Maritzburg), Victor Wanyama (Tottenham Hotspur).