Lechantre atua Bongo kivingine

Sunday August 12 2018

By Charles Abel

Miezi miwili baada ya kuachana na Simba, Kocha Pierre Lechantre amerejea tena nchini ingawa ujio wake ni wa lengo tofauti ambalo halihusiani na klabu hiyo wala nyingine yoyote.
Mfaransa huyo ametua nchini kama mmoja wa maofisa wa idara ya ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) kusimamia mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
UEFA kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) wanadhamini mashindano hayo ambayo ni maalum kwa ajili ya kusaka timu itakayofuzu fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo zitakazofanyika mwakani.
Kocha huyo alianza majukumu yake kwenye mchezo wa timu ya taifa ya vijana wenye umri wa miaka 17 ya Tanzania 'Serengeti Boys' dhidi ya Burundi uliochezwa jana kwenye uwanja wa Taifa jijini.
Katika mchezo huo, Serengeti Boys iliibuka na ushindi wa mabao 2-1

Advertisement