Ngoma apewa program maalumu

STRAIKA mpya wa Azam, Donald Ngoma, amepewa programu maalum nchini Uganda ili aweze kuwa fiti.

Azam iliyoweka kambi nchini Uganda imeendelea na michezo yake ya kirafiki, lakini mchezaji huyo amekuwa pembeni katika michezo hiyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Meneja wa timu hiyo Philip Alando, alisema mchezaji huyo amekwenda Uganda kwaajili ya programu maalum ili aweze kurejea katika hali yake.

"Ngoma huku hajaanza kucheza kweli ila anafanya mazoezi yake ya Gym na uwanjani ili aweze kuwa fiti zaidi, program hii ipo kwa kila mchezaji ili awe fiti," alisema.

Wakati huo huo mchezaji mwingine Yakub Mohammed, ambaye alipata majeraha ya goti tangu mwishoni mwa msimu naye hayupo katika kambi hiyo na alionekana katika mchezo wa Simba dhidi Asante Kotoko.

"Yakub amebaki Tanzania anaendelea na mazoezi kwa kufata utaratibu wa Daktari wake, tukirudi tutaungana nae kwenye maandalizi ya Ligi Kuu," alisema.