VIDEO: Mzee Majuto alikuwa mtu wa watu!

Friday August 10 2018

 

By Rhobi Chacha

Donge Tanga. Sheikh wa Msikiti wa Nuru l hudaa, Rai Rashid Rai amesema Mzee Majuto alikuwa mtu wa kusaidia wakazi wa mji wa Tanga na vijiji vyake, haswa katika masuala ya dini.

Sheikh Rai alisema Mzee Majuto amechangia kiasi kikubwa katika msikiti  unaoitwa Nuru l hudaa uliopo Donge jijini Tanga, karibu na nyumbani kwake kwa kutoa gharama za ramani, na pia ni mwanzilishi wa madrasa kwa kujenga vyumba viwili vya madrasa.

Pia, alisema katika kijiji cha Mabokweni Kiruku ambapo atakazikwa leo kwenye mashamba yake, alitoa eneo lake moja la shamba na kujenga Msikiti wake kwa ajili ya wanakijiji kuswali.

Msikiti huo ambao aliujenga mwaka 2004 na aliumaliza kabla ya mwaka huo kuisha hivyo wanamshukuru kwa kujitolea.

Advertisement