Cannavaro alikubali tizi la Mkongo

Friday August 10 2018

 

By KHATIMU NAHEKA

MENEJA mpya wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' ametua rasmi kuanza majukumu yake na alipoangalia mazoezi hayo akageuka na kusema vijana wameiva.
Cannavaro ambaye amestaafu rasmi soka na kupewa jukumu jipya la kuwa meneja aeta katika kambi ya Yanga juzi usiku.
Cannavaro na jana asubuhi akaanza kazi yake rasmi ya umeneja ambapo alikutana na mtangulizi wake Hafidh Saleh aliyepanda cheo na kuwa Mratibu wa timu hiyo kisha  wakapeana mikakati.
Akizungumza na Mwanaspoti, Cannavaro alisema sasa ameanza kazi rasmi ambapo wiki hii ataitumia kuwa karibu na Hafidh katika kumpa mwongozo wa kazi hiyo.
Mkongwe huyo alisema kwa jinsi alivyoona mazoezi ya jana asubuhi yalitosha kwake kuamini kwamba kwasasa vijana wao wameiva vyema kwa mazoezi waliyoyapata tangu kuanza kwa kambi hiyo.


Advertisement