Buswita abadilishiwa kazi Jangwani

Friday August 10 2018

 

KIUNGO Pius Buswita yeye kambi popote unaambiwa, kwani chini ya Kocha Mwinyi Zahera amekuwa akibadilishiwa nafasi na bado anakinukisha kama kawaida.
Kocha Zahera amembadilishia nafasi kwa mara ya tatu, akimpa majukumu mapya tofauti na ya awali aliyompangia mapema.
Mkongo ameamua kumtumia Buswita kama kiungo mchezeshaji kutoka katikati, tofauti na awali alipoalianza kumtumia kama mshambuliaji wa kati nafasi ambayo alikuwa akiitumikia tangu akiwa chini ya Kocha Mzambia George Lwandamina.
Alipofika Zahera alianza pia kumbadilishia akimtumia kama kiungo mshambuliaji  wa pembeni akicheza hivyo katika mechi mbili za Kombe la Shirikisho Afrika.
Juzi kocha huyo akambadilisha tena kwa kumtumia kama kiungo wa kati mchezeshaji na jamaa akanonekana kuyamudu vyema majukumu hayo.
Katika nafasi hiyo Yanga ilicheza mechi dhidi ya Morogoro Tanzanite Academy na Yanga ikashinda kwa mabao 5-1 huku Buswita akifunga moja ya mabao hayo.

Advertisement