Jamie Vardy aongeza miaka minne Leicester

Friday August 10 2018

 

London, England. Mshambuliaji nyota wa Leicester City, Jamie Vardy, amethibitisha ahadi yake kuwa anataka kudumu katika timu hiyo iliyoandika historia kwa kutwaa ubingwa wa England msimu wa 2016/17 kwa kusaini mkataba mpya.

Vardy ambaye mkataba wake wa awali ulikuwa unamalizika mwishoni mwa mwaka huu, ameongeza miaka minne zaidi hivyo atakipiga kwenye klabu hiyo hadi Juni, 2022.

Vardy, mwenye miaka 31, ameifungia klabu hiyo mabao 88 tangu alipojiunga nayo akitokea Fleetwood Town mwaka 2012  na msimu uliopita alifunga mabao 20.

"Nataka kila mmoja afahamu ninavyojitolea kwa ajili ya klabu hii, ninatamani kubaki na kustaafia soka kwenye klabu hii,” alisema Vardy.

Alisema mkakati wake ni kuhakikisha timu hiyo inarejea mafanikio iliyoyaweka katika Ligi hiyo ilipotwaa ubingwa bila kuatarajiwa.

Advertisement