Mwanamuziki Mwasiti awapa burudani Simba B na Mwadui FC

Wednesday August 8 2018

 

By Charity James

Mkongwe wa HipHop, Rashid Makwiro na mwanadada Mwasiti Almas wamewaburudisha mashabiki wa Simba baada ya kuimba wimbo wao wa hao.

Wakongwe hao katika tasnia ya muziki wamepokewa kwa shangwe na mashabiki wa timu hiyo dakika chache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili cha mchezo wa ufunguzi dhidi ya Simba B na Mwadui FC.

Hadi sasa timu hizo NADP hazijafungana ikiwa ni kipindi cha pili timu zote zinaonekana kushambuliana kwa zamu.

Mashabiki hao walianza kuingia uwanjani mnamo saa 4 asubuhi na wengi wao walikimbilia upande wa majukwaa ya Magharibi iliko skrini kubwa.

Hadi kufikia saa tano, sehemu kubwa ya viti vya majukwaa ya rangi ya kijani, bluu na machungwa ambayo yapo upande huo ilikuwa imejaa.

Hamasa ya mashabiki kuingia uwanjani oliongezeka zaidi pale Bendi ya Muziki wa dansi ya Twanga Pepeta ilipoanza kutumbuiza mnamo saa saba kasoro mchana.

Nje ya Uwanja wa Taifa, umati wa mashabiki umekuwepo hasa kwenye mageti wakiwahi kuingia uwanjani lakini pia wameonekana kwenye misururu mirefu pembezoni mwa Uwanja wa Uhuru na kwenye baadhi ya magari maalum yaliyoandaliwa kuuza tiketi za kuingilia uwanjani

Advertisement